MEZESHA… MEZESHA…

Manzee mezesha moja sitawahi rada ni hii risto ya vile utu umelost kwa society Kenya hii.

Na sitastart kutupia mapolitrickcian blame sababu hiyo mtindo haiwesmake.

Lakini haimaanishi eti hawana blame.

Hebu tucheki risto ya KEMSA ndio tuingize akili.

Ni Kenya tu ndio mawadhii incognito wanaweza kupiga kaletha kwa ofee ya gava na wakalaza tender ya mamita.

Kabla tuanze kumzushia politrickcian, huyu muthii ametudondoa mamita kupitia biarasha ya udingo ni nani?

Sio wewe au mimi?

Jiulize, kama ingekuwa wewe, unge-do?

Just imagine big kahuna fulani wa gava akikuona kando na kukushow uform kampu ya uduu ili muperembe mamita?

Halafu huyu bazenga anakushow eti atakukanja mita rwabe kutoka kwa hiyo storo yote…

Ungeingia boxi au vipi?

Sifichi… Mimi nitachanganyikiwa…

Nitafkiria kuomoka kabla kufikiria storo za waKenya wengine.

Lakini hii fom tumetoa wapi?

Tumeweka ganji mbele ya maisha…

Tuko radhi msee mgonjwa aume pamba ili tuomoke…

Tuko radhi watoi wadedi kwa mikasa ya shule zimejengwa na macontractor mwitu ndio tuingize doo kutoka kwa ganji ya constra…

Tuko radhi maobaro zikuwe makaburi za mandugu zetu ndio tutie ndani niado za wizi.

Lakini hii inakaa farfetched au sio…

Wacha tutoke ‘away’ match ndio tucheze homeground.

Mara ngapi tushakulia vako ganji za job…

Mara ngapi tushadai risiti za vako ili kula doo?

Mara ngapi tushahepa wera tukidai tuko waks lakini tuko side hustle zetu?… Na bado mwisho wa mwezi tunalilia ganji smart?

Kabla kunyooshea mkono wagondi wa KEMSA, tujicheki kama pia sisi tushagondi wengine.

Big Man Yesu alidai eti kabla tudai uchafu kwa macho ya wadhii wengine, tuondoe magongo kwa macho yetu.

#nihayotu